LUGHA

SARUFI: Matumizi Ya Lugha


Sarufi ni sheria, kanuni au taratibu zinastahili kufuatwa katika lugha fulani. Kila lugha huwa na kanuni zake. Katika sarufi tutazingatia sauti(utamkaji), aina ya maneno, upatanisho wa maneo kisarufi, muundo wa sentensi za Kiswahili na kadhalika.
Ufuatao ni mukhtasari wa baadhi ya yale tuliyokuandalia katika matumizi ya lugha. Fungua kila ukrasa ili kusoma mada kwa kina.

Vipashio vya Lugha

Vipashio vya lugha ni viungo mbalimbali vinavyowekwa pamoja katika mpangilio fulani kisarufi, kuunda lugha:

  1. Sauti
  2. Mofimu
  3. Neno
  4. Sentensi
Kwa kuzingatia vipashio hivi vya lugha, tumekuandalia vipengele vifuatavyo katika sarufi:

Aina za Maneno

Kunazo aina nane za maneno ya Kiswahili
Nominomajina, aina za nomino, uundaji wa nomino kutoka kwa maneno mengine, wingi
Vitenzivitendo katika sentensi, aina za vitenzi, mnyambuliko wa vitenzi
Viwakilishimaneno yanayowakilisha nomino; aina za viwakilishi
Vivumishiaina za vivumishi k.v vivumishi vya sifa, n.k
Vielezivielezi halisi, vielezi vya namna n.k
Viunganishia-unganifu, kuonyesha tofauti, sababu, sehemu n.k
Vihisishimaneno ya kuonyesha hisia k.v hasira, mshangao n.k
Vihusishiuhusiano wa nomino na mazingira yake
Kinyumekinyume cha maneno mbalimbali

Muundo wa Maneno

Sauti na Silabiaina za sauti(konsonanti, vokali), silabi, matamshi
Shadda na Kiimbomkazo katika maneno, kiimbo(intonation)
Viambishimaana na aina za viambishi, uainishaji
Mofimumofimo huru, mofimu tegemezi
ViungoMatumizi ya viungo k.v KWA, KU, JI, MA, NI, NA n.k

Upatanisho wa Maneno

Ngelingeli mbalimbali za Kiswahili k.v A-WA, KI-VI n.k
Umoja na Wingiwingi/umoja wa nomino, sentensi n.k
Ukubwa na Udogoonyesha ukubwa/udogo wa neno au sentensi
Nyakati na Halinyakati(uliopita, uliopo, ujao, n.k), NGE, NGALI,
Kukanushakukanusha sentensi katika hali na nyakati mbalimbali


Sentensi

Aina za Sentensichangamano, ambatano n.k
Uchanganuzikikundi nomino, kikundi tenzi n.k
Virai na Vishaziaina za virai, kishazi huru, kishazi tegemezi
Shamirisho na Chagizoshamirisho yamwa, kitondo n.k
Uakifishajialama za kuakifisha k.v swali(?), kikomo (.) n.k

No comments:

Post a Comment