Sunday, June 16, 2013

SARUFI: Matumizi Ya Lugha



Sarufi ni sheria, kanuni au taratibu zinazostahili kufuatwa katika lugha fulani. Kila lugha huwa na kanuni zake. Katika sarufi tutazingatia sauti(utamkaji), aina ya maneno, upatanisho wa maneno kisarufi, muundo wa sentensi za Kiswahili na kadhalika.
Ufuatao ni mukhtasari wa baadhi ya yale tuliyokuandalia katika matumizi ya lugha. Fungua kila ukrasa ili kusoma mada kwa kina.


Vipashio vya Lugha


Vipashio vya lugha ni viungo mbalimbali vinavyowekwa pamoja katika mpangilio fulani kisarufi, kuunda lugha:

  1. Sauti
  2. Mofimu
  3. Neno
  4. Sentensi


Kwa kuzingatia vipashio hivi vya lugha, tumekuandalia vipengele vifuatavyo katika sarufi:

Nominomajina, aina za nomino, uundaji wa nomino kutoka kwa maneno mengine, wingi
Vitenzivitendo katika sentensi, aina za vitenzi, mnyambuliko wa vitenzi
Viwakilishimaneno yanayowakilisha nomino; aina za viwakilishi
Vivumishiaina za vivumishi k.v vivumishi vya sifa, n.k
Vielezivielezi halisi, vielezi vya namna n.k
Viunganishia-unganifu, kuonyesha tofauti, sababu, sehemu n.k
Vihisishimaneno ya kuonyesha hisia k.v hasira, mshangao n.k
Vihusishiuhusiano wa nomino na mazingira yake
Kinyumekinyume cha maneno mbalimbali

Muundo wa Maneno


Sauti na Silabiaina za sauti(konsonanti, vokali), silabi, matamshi
Shadda na Kiimbomkazo katika maneno, kiimbo(intonation)
Viambishimaana na aina za viambishi, uainishaji
Mofimumofimo huru, mofimu tegemezi
ViungoMatumizi ya viungo k.v KWA, KU, JI, MA, NI, NA n.k

Upatanisho wa Maneno

Ngelingeli mbalimbali za Kiswahili k.v A-WA, KI-VI n.k
Umoja na Wingiwingi/umoja wa nomino, sentensi n.k
Ukubwa na Udogoonyesha ukubwa/udogo wa neno au sentensi
Nyakati na Halinyakati(uliopita, uliopo, ujao, n.k), NGE, NGALI,
Kukanushakukanusha sentensi katika hali na nyakati mbalimbali

Sentensi


Aina za Sentensichangamano, ambatano n.k
Uchanganuzikikundi nomino, kikundi tenzi n.k
Virai na Vishaziaina za virai, kishazi huru, kishazi tegemezi
Shamirisho na Chagizoshamirisho yamwa, kitondo n.k
Uakifishajialama za kuakifisha k.v swali(?), kikomo(.) n.k

No comments:

Post a Comment